Mkurugenzi wa CIA William Burns amesema kuwa kunahitajika kusitishwa kwa mapigano ili kuwapa watoto wanaokabiliwa na njaa huko Gaza msaada unaohitajika wa kibinadamu huku Israel ikiendelea na mashambulizi dhidi ya eneo la Palestina.
“Ukweli ni kwamba kuna watoto wanaokufa kwa njaa. Wana utapiamlo kutokana na ukweli kwamba msaada wa kibinadamu hauwezi kuwafikia. Ni vigumu sana kusambaza misaada ya kibinadamu kwa ufanisi isipokuwa uwe na usitishaji vita,” alisema Burns wakati kikao cha Kamati ya Ujasusi ya Seneti.
Alisema mkataba unaosubiriwa wa kuachiliwa kwa mateka kati ya Israel na Hamas ambao hapo awali utaruhusu usitishaji mapigano kwa muda na kuwawezesha watu kupata msaada unaohitajika sana wa kibinadamu una “thamani kubwa.