Katika mashindano ya Marathon ya Berlin 2023 yaliyofanyika tarehe 24 mjini Berlin, Ujerumani, mchezaji maarufu wa mbio za masafa marefu wa Kenya Eliud Kipchoge alipata ubingwa kwa kutumia saa 2 dakika 2 na sekunde 41.
Hii ni mara yake ya tano kupata ubingwa kwenye Mashindano ya Marathon ya Berlin.
Mchezaji wa Ethiopia Tigist Assefa naye amevunja rekodi ya dunia na kujinyakulia ubingwa kwenye mashindano hayo kwa upande wa wanawake kwa kutumia saa 2 dakika 11 na sekende 52.
“Haikwenda kama ilivyotarajiwa lakini ndivyo michezo ilivyo,” Kipchoge alisema baada ya mbio hizo, akikiri kwamba alidhani angevunja rekodi ya dunia.
“Nimejifunza masomo mengi. Nimeshinda lakini sijavunja rekodi ya dunia. Kila mbio ni somo la kujifunza.”
Kuhusiana na matarajio ya kutetea taji lake la Olimpiki, alisema matokeo ya Berlin Marathon hayana uhusiano wowote na mipango yake na kwamba “ataweka uzoefu wangu wote mwakani kwenye Olimpiki huko Paris, na kujaribu kuwa mwanadamu wa kwanza kushinda. kwa mara ya tatu katika historia”.