Mbunge Halima Mdee amemuomba Waziri wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kueleza msimamo wa Serikali kuhusu ujenzi wa mradi wa New Kawe City uliosimama tangu mwaka 2017.
Mdee ameyasema hayo leo May 26, 2021 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka 2021/22
“Kuna wananchi wamewekeza zaidi ya BILIONI 3 wameshanunua nyumba kabla hazijajengwa Waziri unatuambia kuna Crisis, Tafiti zinaonyesha tuna upungufu wa zaidi ya nyumba MILIONI 3 na kila mwaka nyumba laki mbili zinahitajika halafu mnakaa hapa mnasema hatuna mapato” Mdee
“Wakati pale Kawe New City iliyokuwa inatarajiwa kuwa na wakazi 50,000 ingekuingizia Property Tax mpaka ungekimbia, kwa nini tunafikiria kimaskini? tusipotekeleza huu mkataba mnaenda kulipa BILIONI 100 kwa mkandarasi kwa kuvunja mkataba, hii ni akili au nini, nitaomba Waziri unipe majibu kwa maslahi ya watu wa Kawe” Mdee