“Ni sahihi kweli mwananchi akienda hospitali akiwa hana pesa hakuna mahali kitu chochote anaweza kufanya na matokeo yake anaenda kukabiliana na kifo, hakuna Mbunge aliyetumwa sukari wala nyama hapa. Hali za wananchi wetu ni mbaya na tatizo lao ni dawa, Serikali haiwezi kufilisika kwa kuwapatia matibabu bure wananchi wake”- Mbunge wa Kamaha Mjini Jumanne Kishimba
“Kuna hili suala la bima za afya mtu anakwenda hospitali na kuambiwa dawa hakuna, kwanini Waziri Simbachawene asipunguze Askari traffic barabarani na atuhamishie baadhi ya Polisi hospital ili mgonjwa anapokuwa na bima kisha akaambiwa hakuna dawa aende akaripoti kwa Polisi kwa lengo la kunusuru roho yake”-Mbunge wa Kamaha Mjini Jumanne Kishimba