Katibu Mkuu wa Jumyiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa Fakii Raphael Lulandala (MNEC) amepokelewa katika Ofisi ndogo za Makao makuu ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana Upanga Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Oktoba, 2023 ambapo amewataka watendaji wa jumuiya hiyo ngazi za mikoa na wilaya kutimiza majukumu waliyoaminiwa na kupewa.
Lulandala amesema hayo katika mkutano wa wakuu wa Idara za UVCCM Taifa, Watumishi wa Ofisi Ndogo Makao Makuu Upanga, Makatibu wa UVCCM Mikoa yote, baadhi Wenyeviti Mikoa Jirani,Makatibu wa Wilaya pamoja na Wanachama wa UVCCM na CCM Mkoa wa Dar es Slaam na mikoa Jirani.
Mapokezi hayo yameongozwa na mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa Mohammed Ali Kawaida (MCC) na makamu mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Rehema Sombi.