Stori kutoka Mahakama ya KISUTU Dar es Salaam ziliingia kwenye Headlines za vyombo vya Habari mfululizo baada ya Mahakama hiyo kuahirisha kusoma hukumu ya Mawaziri wawili wa zamani, Basil Pesambili Mramba, Daniel Yona na Gray Mgonja ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Hazina kwa mara mbili mfululizo kutokana na sababu mbalimbali.
Leo July 06 2015 imesikika tena toka Mahakamani hapohapo, Hukumu imetolewa… Basil Mramba na Daniel Yona wamekuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela pamoja na faini ya Milioni 5 kila mmoja, alafu Grey Mgonja ameachiwa huru baada ya Mahakama kumwona hana hatia.
Breaking: Mawaziri wa zamani,Basil MRAMBA (Wizara ya Fedha), Daniel YONA (Nishati na Madini) wamehukumiwa kifungo cha Miaka mitatu jela.
— millard ayo (@millardayo) July 6, 2015
#Tweet2: Hukumu hiyo ni pamoja na faini ya Mil. 5 kila mmoja. Hukumu imetolewa Mahakama ya KISUTU leo JULY 6 2015 muda mfupi uliopita.
— millard ayo (@millardayo) July 6, 2015
#Tweet3: Daniel YONA na Basil MRAMBA wamekutwa na Hatia ya kuisababishia hasara Serikali pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.
— millard ayo (@millardayo) July 6, 2015
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.