Kwenye miaka ya karibuni tumeona kufunguliwa kwa idadi kubwa ya sehemu za kufanyia mazoezi (gym) na pia tumeona idadi kubwa ya Watu wakifanya mazoezi kwa wingi viwanjani, barabarani au mitaani hasa mijini ambapo Wataalamu wanasema ni kutokana na miili kuongezeka kwa wengi huku aina ya vyakula ikiwa moja ya sababu.
Sasa utafiti ambao tumeunyaka ni kwamba kunayo hatari kwa Watu wenye vitambi ambapo kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa na BMJ huko Uingereza, Binadamu kuwa na kitambi kilichozidi kiasi kunapelekea kuwa na hatari ya kufariki haraka.
Kufariki huko haraka kutatokea pale Mtu mwenye kitambi anapopata maradhi mbalimbali hivyo Watu inabidi wawe makini, kwa Wanawake kila centimeter 10 za ongezeko la kitambi huongeza hatari ya kifo cha mapema kwa asilimia nane.
Utafiti huo wa BMJ umeeleza pia kwamba kwa upande wa Wanaume kila centimeter kumi za ongezeko la kitambi zinaongeza hatari ya kifo cha haraka pindi wanapougua kwa asilimia kumi na mbili hivyo Watu wasifuge vitambi ni hatari kwa afya, umesisitiza utafiti huo.