Habari kubwa Tanzania kwa sasa ni jinsi gani Watanzania wataweza kuchangia matibabu kwa ajili ya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba na kumekuwa na mawazo mengi ila wazo lililokuwa kichwani mwa wengi ni kufanyika tamasha ili hela zitakazopatikana zitumike kwa matibabu.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Mtangazaji wa Efm Maulid Kitenge amepost post akiwa na C.E.O wa Clouds Media Group Kusaga na kuandika hivi “Nimekutana na Joseph Kusaga hapa New York, Marekani leo na ameniambia wamelipokea wazo la baadhi ya wasanii kufanya Matamasha matatu katika mikoa mikubwa kama Dar, Arusha na Mwanza kwa ajili ya kuchangia matibabu ya ndugu yetu Ruge Mutahaba”
RPC ALIEONDOLEWA MWANZA AZUNGUMZA “PASHA KWA KUNIONDOA SALAMA”