Kituo kwa ajili ya kuwanoa wanawake wakiwemo viongozi Wanawake nchini kimezinduliwa leo jijini Dar es salaam, lengo likiwa ni kuwapa Wanawake haki ya kupona na kupumzika bila kupingwa na kupata utulivu na amani ya moyo kutokana na makovu yanayosababishwa na mifumo kandamizi.
Kituo hiki ambacho kinaitwa Nendiwe Feminist and Coaching Center kimeanzishwa na Wanawake kwa ajili ya Wanawake Viongozi wa Sekta mbalimbali na kimeshaanza kazi ya kuwanoa Viongozi wa kike Vijana, malengo ya kituo hiki ni sehemu salama (safe space) , elimu na kujikutanisha na kujikubali kama Wanawake.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Mwanzilishi mwenza wa kituo Mary Rusimbi amesema “Hii ni sehemu iliyotengenezwa na Wanawake kwa ajili ya Wanawake kwa ajli ya ustawi wetu, tuna mikwaruzano mbalimbali maishani , mifumo kandamizi inayotufanya tuwe na makovu”
Mfemenia mbobevu na Mkurugenzi Mkuu wa Hope Afrika kutoka nchini Zimbabwe, Hope Chigundu ni Mgeni wa heshima kwenye uzinduo huo ambapo amesema vituo kama hivyo ni muhimu wana kwa ustawi wa Wanawake