Kiungo wa kati wa Manchester United Kobbie Mainoo ameitwa kwa mara ya kwanza katika timu ya taifa ya Uingereza kabla ya mechi zao mbili za kirafiki, timu ya taifa ilisema Jumanne, baada ya kinda huyo kufanya vyema katika klabu hiyo ya Ligi ya Premia.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18, ambaye awali alikuwa sehemu ya kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 21 kwa ajili ya kufuzu kwa U-21 Euro 2025 mwezi huu, amejumuishwa katika timu ya meneja Gareth Southgate kwa mechi zitakazochezwa Wembley dhidi ya Brazil Machi 23 na Ubelgiji Machi 26.
Mainoo ni mhitimu wa akademi ya vijana ya United na amecheza mechi 14 kwenye kikosi hicho cha Old Trafford kwenye Ligi ya Premia msimu huu.
“Ni heshima kupokea mwito wangu wa kwanza,” Mainoo alichapisha kwenye Instagram.