Kiungo wa kati wa Manchester United Casemiro huenda asicheze kabla ya Krismasi baada ya kupata jeraha la misuli ya paja.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil alitolewa wakati wa mapumziko katika kipindi cha kipigo cha 3-0 cha United dhidi ya Newcastle kwenye Kombe la Ligi wiki iliyopita.
Hapo awali United walisema angekuwa nje ya uwanja kwa “wiki kadhaa,” lakini siku ya Jumanne meneja Erik ten Hag alitoa dalili wazi ya ni muda gani itamchukua Casemiro kupona.
Akizungumza kabla ya mechi ya Ligi ya Mabingwa ya United dhidi ya Copenhagen siku ya Jumatano, Ten Hag alisema Casemiro na (Lisandro) Martinez walikuwa na “majeraha makali sana” na kuongeza, “Sitarajii warudi kabla ya Krismasi.”
Martinez ambaye hayupo kwa muda mrefu ana jeraha la mguu.
United ina mechi 10 katika mashindano yote kati ya sasa na Krismasi na pia haina mabeki Luke Shaw na Tyrell Malacia waliojeruhiwa.
“Nina ratiba za muda,” Ten Hag alisema. “Lakini daima ni vigumu kutayarisha (nyakati za kurejesha) … kwa sababu kunaweza kuwa na vikwazo wakati wa kipindi cha ukarabati.”
Kikosi cha United cha Copenhagen pia kinajumuisha Victor Lindelof na Marcus Rashford, ambao walikosa mchezo wa Jumamosi dhidi ya Fulham kutokana na ugonjwa na tatizo la mguu mtawalia, lakini Ten Hag alisema walikuwa “100%.