Kiungo wa kati wa Tottenham kutoka Mali, Yves Bissouma atakosa kuanza kwa msimu wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kusimamishwa na klabu hiyo kufuatia uchunguzi wa picha zinazomuonyesha akivuta nitrous oxide, au laughing gas.
Wikiendi iliyopita, Bissouma aliupload klipu kwenye mtandao wa kijamii wa Snapchat ambapo alionyesha akitumia nitrous oxide, ambayo sasa ni dawa ya daraja la C chini ya sheria za Uingereza.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Mali aliomba msamaha na kukiri “kutokuwa na uamuzi mkubwa” katika taarifa yake.
Kufuatia uchunguzi, Bissouma alipigwa marufuku ya mechi moja, kumaanisha kuwa atakosa mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu ya Tottenham Jumatatu huko Leicester.
“Yeye ni mwanasoka wa klabu hii – ana majukumu kwa klabu, wachezaji wenzake, wafuasi wetu, kila mtu anayehusishwa na klabu, na ameshindwa katika majukumu yake,” meneja wa Tottenham Ange Postecoglou alisema Alhamisi.
“Hatakuwepo Jumatatu… lakini zaidi ya hapo, kuna kazi pia ya kufanywa juu ya uaminifu kati yangu na Biss, na kati ya Biss na kundi. Hilo ndilo analopaswa kulifanyia kazi ili kurejesha uaminifu huo. ”
Nitrous oxide hutumiwa kimatibabu kama anesthetic na painkiller. Lakini watu pia huitumia kupata juu. Matumizi makubwa yanaweza kuharibu tishu za ubongo na neva.