Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, ameuagiza uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mkoa wa Geita, kuhakikisha unasimamia kwa karibu uendeshaji wa kivuko cha Mv Chato II, hapa kazi tu, ili wananchi wa Mkoa huo waweze kufaidi matunda ya Serikali kwa maendeleo yao binafsi na nchi nzima kwa ujumla.
Akizungumza wakati wa kupokea kivuko hicho wilayani Chato mkoani Geita, Waziri Chamuriho, amsema kuwa kivuko hicho ambacho kimepokelewa leo kitatumika kwa muda na pindi uongozi husika utakapojiridhisha na ufanisi wake, utakuja tena kukizindua rasmi.
“Kama mnavyoona leo hii tumekipokea kivuko hiki ambacho tutakiangalia ufanisi wake kwa muda, tukiridhika tutakuja kukizindua, hivyo wananchi wa hapa tunaomba mkitunze kwa ajili ya maendeleo yenu na nchi kwa ujumla”, Waziri Chamuriho.
Chamuriho, amesisitiza kuwa katika kuhakikisha usalama wa vivuko vyote nchini, Serikali itaendelea kuboresha usimamizi wa uendeshaji wa vyombo vya majini ili kuepusha matukio ya ajali yanayoweza kutokea.
Aidha, Chamuriho ameuelekeza Wakala wa Meli nchini (TASAC), kuendelea kutoa mafunzo kwa wamiliki na waendesha vyombo vya usafiri majini ikiwemo TEMESA ili kuwaongezea ufahamu juu ya umuhimu wa kuzingatia taratibu na kanuni zinazosimamia uendeshaji wa vitu hivyo.
Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Mhandisi Japhet Maselle, amesema kuwa kivuko hicho kilianza kujengwa rasmi mwezi May, 2019 na Mkandarasi mzawa kampuni ya Songoro Marine Transport.
Ameongeza kuwa kivuko hicho kina uwezo wa kubeba Tani 100 ambapo sawa na magari madogo 10 pamoja na abiria 200 na kimefungwa injini mbili mpya na tayari kimeshafanyiwa ukaguzi na kusajiliwa na TASAC.
“TUNAANZA KUGOMBANA, CCM MSIPENDELEE” MAALIM SEIF AGEUKA MBOGO MBELE YA MA-RC, DC