Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dastan Kitandula amesema Watu wategemee makubwa baada ya kufanya ukaguzi wa maandalizi ya mwisho ya maonesho ya Swahili International Tourism Expo 2023 yanayotarajiwa kufanyika kuanzia October 6 mpaka October 8 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City Dar es salaam.
Naibu Waziri Kitandula amesema kuna mengi mazuri ya utofauti mwaka huu kwasababu kutakuwa na maonesho ya wanyama wa mbugani kabisa pamoja na mengine yanayopatikana katika Vivutio vya Kitalii “Watu wategemee makubwa, tumekuja kufanya ukaguzi wa maandalizi na ninafurahi kusema yako vizuri sana, ni zaidi ya 96% yamekamilika, miaka mingine kulikuwa hakuna wanyama ila mwaka huu watakuwepo”