Kiwango cha umaskini kimeelezwa kupungua katika maeneo yote (Mijini na Vijijini), ambapo Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango amesema, umaskini umepungua Mijini kutoka 21.7% hadi 15.8% na maeneo ya vijijini umepungua kutoka 33.3% hadi 31.3%”.
Hayo ameyasema leo Juni 11, 2020 na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, wakati akisoma bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2021/20 bungeni Dodoma.
“Hadi Aprili 2020 Jumla ya viwanda vipya 8,477 vimeanzishwa nchini, ongezeko hili la viwanda limeongeza utoshelevu wa bidhaa nchini, mathalani uwezo wa uzalishaji wa Saruji umeongezeka kutoka Tani Mil 4.7 2015 hadi Tani Mil 9. 1 mwaka 2019” Mpango
“Hadi Aprili 2020, Serikali imeboresha miundombinu ya huduma za afya kwa kujenga Zahanati 1,198, Vituo vya Afya 487, Hospitali za Halmashauri 71, za Rufaa 10, za Kanda 3, kuongezeka kwa Bajeti ya vifaa na dawa kutoka Bil 31, 2015 hadi Bil 269 2019” Mpango
“Hadi Aprili 2020 akiba ya fedha za kigeni ilifikia Dolla za Marekani Bil 5.3, kiasi hiki kinatosheleza mahitaji ya fedha za kigeni ya kuagiza bidhaa nje ya nchi kwa kipindi cha miezi 6 ukilinganisha na Dolla Bil 4.4 cha mwaka 2015” Mpango
“Ukuaji wa Pato la Taifa unatarajiwa kupungua kutoka maoteo ya awali ya 6.9% na kufikia 5.5% mwaka 2020 ikilinganishwa na 7% mwaka 2019. Hii ni kutokana na mvua nyingi ambazo zimeharibu miundombinu ya usafirishaji nchini na athari za ugonjwa wa COVID–19” Mpango