Kulingana na ripoti iliyotolewa na Ofisi ya Sensa ya Marekani, kiwango cha umaskini nchini humo kilipanda hadi asilimia 12.4 mwaka 2022, huku umaskini wa watoto ukiongezeka maradufu kutoka 2021.
Kipimo cha Kuongezeka Umaskini (SPM) ambacho kinapima iwapo watu wana rasilimali za kutosha kukidhi mahitaji yao kiliongezeka kwa asilimia 4.6 mwaka 2022 kutoka mwaka wa nyuma yake.
Takwimu hizo pia zilionyesha kuwa kiwango cha umaskini wa watoto kiliongezeka zaidi ya mara mbili, kutoka asilimia 5.2 mwaka 2021 hadi asilimia 12.4 mwaka 2022.
Ni mabadiliko makubwa zaidi kwa umaskini wa watoto tangu shirika hilo lianze kufuatilia kipimo hicho mwaka 2009.
Kwa mujibu wa Kituo cha Vipaumbele vya Bajeti na Sera, taasisi ya washauri bingwa wa mrengo wa kushoto ya Marekani, ongezeko la umaskini linamaanisha ongezeko la Wamarekani milioni 15.3 wanaoishi katika umaskini.
Rais wa Kituo cha Vipaumbele vya Bajeti na Sera Sharon Parrott amesema katika taarifa kwamba kupanda kwa kiwango cha umaskini, ambacho ni kikubwa zaidi katika rekodi ya zaidi ya miaka 50 kwa ujumla na kwa watoto, kunasisitiza jukumu lililopo kwenye uchaguzi wa sera katika kiwango cha umaskini na ugumu wa maisha nchini.