Leo August 04 2016 Naibu waziri wa mazingira na muungano kutoka ofisi ya makamu wa Rais, Luhaga Mpina akiambatana na baadhi ya viongozi wa NEMC kanda ya mashariki walifanya ukaguzi kwenye viwanda vya nguo vya Urafiki na NIDA.
Kwenye kiwanda cha NIDA Tabata wamekuta mazingira si rafiki ambapo maji yatokayo kiwandani yanaenda kwenye mto kibangu unaopita Tabata jijini Dar es salaam. Hivyo Serikali imekipiga faini ya milioni 30 kiwanda cha NIDA baada ya kuvunja sheria ya mazingira kwa kutiririsha maji hayo katika mto kibangu na wametakiwa kulipa ndani ya siku saba.
ULIKOSA HII YA MILIONI 45 ZILIVYOWATOKA WATU WA KIWALANI HIVIHIVI KISA CHEMBA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI