Leo January 3, 2018 Tukiwa tumeanza mwaka mpya kila mmoja amejipanga kwa aina yake katika mwaka nikusogezee hii kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje, Harry Kalaba, ametangaza kujiuzulu wadhifa wake, kwa kile alichodai kushindwa kwa Rais wa Zambia Edgar Lungu, kupambana na rushwa.
Amesema tayari amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais Lungu na kwamba amechukua uamuzi huo kwa moyo mzito, hata hivyo Msemaji wa Rais, Amos Chanda, amesema Ikulu bado haijapokea barua ya kujiuzulu kwa Kalaba.
Kalaba anakuwa Waziri wa tatu kuondoka ndani ya serikali ya Rais Lungu baada ya kutimuliwa kwa Mawaziri wawili akiwemo Waziri wa Mipango na Waziri wa Habari na Utangazaji.
Kalaba, ambaye ni Mbunge wa chama tawala cha Patriotic Front (PF), anatajwa kuwa mgombea wa urais katika uchaguzi wa urais utakaofanyika mwaka 2021 ikiwa Lungu atajiweka pembeni.
KAULI YA CHADEMA TOKA NAIROBI KUHUSU MKE WA KENYATTA KUCHANGIA MATIBABU YA LISSU
VIDEO: GOOD NEWS: JPM ATANGAZA KUTOA TSH BILIONI 200