May 12. 2018 Naibu Spika Dr Tulia Ackson alikuwa mgeni rasmi katika semina ya Wanafunzi wa chuo kikuu Dodoma (UDOM) iliyofanyika katika ukumbi wa Chimwaga lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kubadilisha fikra na kutimiza wajubu wao katika sekta ya elimu na jamii kwa ujumla.
Dr Tulia amesema >>>”Sisi kama vijana lazima tuwe ni watu wenye nidhamu katika mambo tunayoyafanya, mfano mdogo wewe kama mwanafunzi unaingia darasana na umekuta tayari mwalimu ameingia darasani na bado unaona ni kawaida. Ukizoea kuchelewa darasani utaona ni kawaida kuchelewa kwa kila jambo“
“Hutu tusababu tudogo ndio tunatusumbua sisi kama vijana, kutunza muda ni muhimu sana. Muda unaopanga kufanya jambo Fulani usiutumie kufanya jambo lingine fanya lile ulilokuwa umelipanga” –Dr Tulia
“Kama kijana unafika mahali unakaa siku nzima huelewi siku hiyo unataka kufanya nini, hapa niongee kiingereza kidogo Your a problem (wewe ni tatizo) sio kwamba una matatizo lakini wewe ndio tatizo” –Dr Tulia
“Jamani Magufuli ataimba, kila siku anabadilisha sheria IKULU” –Hussein Bashe