Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akiwa mkoani Dodoma amesema Serikali itazichukulia hatua shule zote zitakazoshindwa kuwahakikishia hali ya usalama wanafunzi wake ikiwemo matukio ya udhalilishaji ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara.
“Serikali haiwezi kuvumilisha shule ambazo hazihakikishii watoto usalama wao, niwahakikishie watanzania kwamba Serikali itachukua hatua kali kwa yeyote yule anayefanya vitendo vya kuwazalilisha watoto shuleni. ” –Prof Joyce Ndalichako
Masauni VS Joshua Nassari kuhusu mwanamke aliyejifungulia kituo cha Polisi