Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ametoa utabiri wake kuhusiana na majibu ambayo Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Askofu Zakaria Kakobe atawapa Mamlaka ya Mapato (TRA) kuhusu mali na utajiri wake.
Kupitia katika ukurasa wake wa Twitter Lema ametweet hivi namnukuu “Majibu ya Askofu Kakobe kwa TRA ni haya yafuatayo kuhusu utajiri wake kuliko Serikali….
Hagai 2:8. Fedha ni mali yangu na dhahabu ni mali yangu asema Bwana wa Majeshi.
Zaburi 24:1. Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana ,Dunia na wote wakaao ndani yake.” – Lema
Majibu ya Askofu Kakobe kwa TRA ni haya yafuatayo kuhusu utajiri wake kuliko Serikali….
Hagai 2:8. Fedha ni mali yangu na dhahabu ni mali yangu asema Bwana wa Majeshi.
Zaburi 24:1. Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana ,Dunia na wote wakaao ndani yake.
— Godbless E.J. Lema (@godbless_lema) December 30, 2017
“KAKOBE ASIFANYE KANISA LAKE KICHAKA CHA KUFANYIA SIASA” -Rc. Gambo, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA