Habari kutoka Mbagala Charambe leo March 6, 2018 ni kwamba zaidi ya vibanda 600 katika soko la Mkochela, vimeungua moto alfajiri ya leo na chanzo cha moto kinasadikiwa kuwa ni hitilafu ya umeme.
Afisa Habari wa Jeshi la Zima Moto Dar es Salaam Peter Mwambene ameeleza kuwa kwa mwaka huu hii ni mara ya pili, mwingine ulitokea mwezi February na sababu ya moto huu imekuwa ile ile kwa awamu zote mbili.
BARUA YA HUSSEIN BASHE KWA BUNGE “UMOJA, USALAMA TAIFA”, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA NA KUSIKILIZA