Stori ambayo nisingependa uikose leo March 6, 2018 ni kutoka Zimbabwe ambapo taifa hilo linaungana na mataifa mengine kupiga marufuku kuingizwa kwa vyakula vya nyama kutoka nchini Afrika Kusini.
Hatua hii inakuja baada ya kuzuka kwa maambukizi ya backteria ya listeria vilivyobainika katika vyakula hivyo ambavyo ni hatari kwa matumizi ya binadamu.
Serikali ya Afrika Kusini imepiga marufuku uuzwaji wa sausage inayofahamika kama Polony, na kutoa wito kwa watu kutokula bidhaa hiyo.
Ripoti zinasema kuwa watu 180 wamepoteza maisha kwa kula bidhaa hiyo iliyokuwa na sumu. Wamiliki wa maduka yanayouza Sausage hizo, wamelazimika kuziondoa baada ya tangazo hilo.
BARUA YA HUSSEIN BASHE KWA BUNGE “UMOJA, USALAMA WA TAIFA”, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA NA KUSIKILIZA