Leo February 25, 2018 Rais John Magufuli ameungana na waumini wa Parokia Teule ya Mlimani iliyopo Chato mkoani Geita kusali ibada ya Dominika ya pili ya Kwaresma huku akichangia Shilingi Milioni 2 kwa ajili ya ujenzi unaoendelea kanisani hapo.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawsiliano ya Rais imesema Parokia Teule ya Chato imepandishwa hadhi kutoka kilichokuwa Kigango cha Mlimani na hivi sasa waumini wanaendelea kukamilisha majengo ikiwemo nyumba ya Paroko kabla ya kusimikwa rasmi kuwa Parokia.
Akitoa salamu baada ya ibada hiyo, Rais Magufuli amewapongeza waumini wa Parokia hiyo kwa juhudi walizofanya kujenga Kanisa la Parokia hiyo.
Katika taarifa hiyo, Rais amemshukuru Askofu wa Jimbo Katoliki Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi kwa kukipandisha hadhi kigango cha Mlimani kuwa Parokia.
“Pamoja na kujenga Parokia yetu tuendelee kuliombea Taifa letu na kujiweka tayari katika maisha ya Duniani,” Rais Magufuli.
RPC Kinondoni amezungumza kuhusu Majeruhi wa Risasi waliopo OYSTERBAY Polisi