Kulikuwa na taarifa kuwa Benki ya Dunia (WB) huenda ikasitisha mkopo wake kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ungesaidia ujenzi wa Barabara ya njia sita kutoka Kimara hadi Pwani.
Leo February 7, 2018 Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas amesema kuwa taarifa hizo serikali haijazipata na kueleza kuwa fedha zinazotumika kwenye ujenzi huo ni za serikali. Pia amegusia ujenzi wa barabara ya juu TAZARA
“Ujenzi wa barabara ya juu TAZARA umefikia asilimia 70 na itaanza kutumika mwaka huu, Ujenzi wa barabara za juu Jijini Dar es Salaam pia utaanza katika makutano ya barabara maeneo ya Chang’ombe, Uhasibu, Kamata, Moroko, Mwenge, Magomeni na Tabata”-Dr. Hassan Abbasi
“HALI NI MBAYA KULIKO ILIVYOKUWA MWANZO” -NAPE NNAUYE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA