Leo October 29, 2018 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa kuanzia leo siku ya Jumatatu hadi Jumapili anapokea taarifa yoyote za majina ya watu wanaofanya vitu kinyume na maadili ya kitanzania yakiwemo ya ushoga na wanaojiuza kwa njia ya mtandaoni.
Hata hivyo RC Makonda amesema kuwa Amber Rutty ambaye hivi karibuni picha zake za utupu zimevunja mtandaoni na mpenzi wake wapo chini ya ulinzi wa Polisi.
“Tayari Amber Rutty na Bwana yake wapo chini ya Polisi, pia nimepata taarifa kuwa kuna mashoga kazi yao kujinadi mitandaoni, kuanzia leo Jumatatu hadi Jumapili napokea taarifa ya jina lolote la anayefana vitendo kinyume na maadili ya kitanzania, yapo makundi mengine WhatsApp kazi yake kuhamasisha tendo la ngono, tumeamua kulivalia njuga suala la makosa ya kimtandao” RC Makonda.
Alichozungumza RC Makonda kwenye ibada ya kuaga mwili wa maremu Isaac Gamba, Bonyeza play hapa chini kutazama