Kanisa la Kianglikana Tasmania lina mpango wa kuuza makanisa 78 kati ya makanisa yake 133 ili kusaidia kuwalipia walionyanyaswa kijinsi walipokuwa watoto.
Waumini wa jimbo hilo kusini mwa Australia wamekasirishwa na hatua hiyo ya kuyapoteza makanisa hayo ambayo yana zaidi ya miaka 130, lakini manusura wamesema hatua hiyo ni ujumbe muhimu wa kupata msahama kutoka kwa Mungu.
Kasisi mkuu wa Tasmania, Richard Condie amesema ‘ uchungu’ wa kuyauza makanisa hayo ni hatua ambayo itawapatia manusura wote wa unyanyasaji wa kingono haki.
Zaidi ya malalamishi ya 1,100 ya visa vya unyanyasaji wa kingono vimeripotiwa dhidi ya kanisa hilo la Australia. Madai hayo yameorodheshwa kutoka kwa mwaka wa 1980 hadi 2005 na yametajwa dhidi ya makanisa 569, yakiwajumuisha wahubiri 247.