Kero ya foleni si Dar es salaam tu, hii imekuwa ni kero kwenye miji mingi duniani, London pia inatajwa kuwa na tatizo kubwa la foleni ambapo ripoti mbalimbali zinaeleza kuwa abiria kwa wastani anatumia masaa 101 akiwa kwenye foleni kila mwaka London.
Ufumbuzi wa tatizo hili umefanyika kwenye nchi mbalimbali ikiwemo maboresho ya barabara, kuwepo kwa treni na mabasi ambapo wananchi wengi hutumia usafiri wa umma lakini hawa jamaa kutoka kwenye kampuni moja huko London wamekuja na wazo ambapo wamependekeza magari yatengenezewe barabara za chini ya ardhi.
ULIKOSA? Tamko la Polisi DSM kuhusu wanaoosha magari barabarani wakati wa foleni…Bonyeza play hapa chini