Leo January 2, 2018 nikusogezee stori kutoka kwa jirani zetu wa Kenya kwa Rais Uhuru Kenyatta ambapo Wapangaji wa nyumba katika mtaa wa Lang’ata jijini Nairobi, ambao wamekataa kulipa kodi iliyoongezwa na mwenye nyumba wao wamepata mshtuko mkubwa baada ya mwenye nyumba kumwaga kinyesi ndani ya nyumba zao.
Wapangaji 40 wa nyumba zinazoitwa Ocean Park Apartments walienda mahakamani kutafuta msaada ili kuzuia mwenye nyumba yao kupandisha kodi na mahakama ikaamua waendelee kulipa Tsh. 540000 kila mwezi ambayo walikuwa wakilipa awali.
Mwenye nyumba hizo anayefahamika kwa jina Joseph Kagwatha alikuwa amewafahamisha wapangaji wake kuhusu kodi mpya na ilitarajiwa walipe Tsh. 650000 kutoka Tsh. 540000 kila mwezi, lakini wapangaji waligoma.
Baada ya mgogoro baina yao kuibuka, Kagwatha alikata huduma muhimu kwenye nyumba hizo kama maji na umeme na kusimamisha huduma za ukusanyaji taka.
Mahakama ilimwambia mwenye nyumba, nanukuu “Unashauriwa kurejesha huduma zote kwa mfano maji, umeme, ukusanyaji taka, ulinzi, na huduma za uegeshaji magari mara moja,”
Licha ya amri ya Mahakama, mwenye nyumba ameripotiwa kutumia kinyesi cha binadamu ili kuwafukuza wapangaji wake, hali ambayo imekuwa hatari kwa maisha ya wapangaji hao.
UAMUZI WA TCRA KWA VYOMBO VYA HABARI VILIVYOKIUKA KANUNI ZA UTANGAZAJI
VIDEO ILIYOWANASA BABU SEYA NA WANAE WAKIINGIA IKULU LEO