June 24 2016 Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ‘TAMISEMI’ imetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2016. Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali.
Jumla ya wanafunzi 65,720 wakiwemo wasichana 29,457 na wavulana 36,263 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi. Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 34,064 wakiwemo wasichana 13,466 na wavulana 20,598 sawa na asilimia 52 watajiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati.
Wanafunzi 30,897 wakiwemo wasichana 15,445 na wavulana 15,452 sawa na asilimia 47 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara na wanafunzi 759 wakiwemo wasichana 220 na wavulana 539 sawa na asilimia 1 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya Ufundi.
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2016 wataanza muhula wa kwanza July 11 2016 na hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya shule.
Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati, endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti July 24 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kuripoti nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi………kuyatazama bonyeza hapa
ULIKOSA HII YA RAIS MAGUFULI ALIPOSEMA UNAPOKWISHA UCHAGUZI UNAKUWA WAKATI WA KAZI, HAIWEZEKANI KILA SIKU SIASA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB INSTAGRAM YOUTUBE