Napoli wamekana kufahamu kuhusu midoli wanaofanana na mshambuliaji nyota Victor Osimhen na wanatishia kuwashtaki watengenezaji wa midoli hiyo.
Napoli wamekuwa wakitaka kujitenga na aina yoyote ya kejeli dhidi ya Osimhen na wamekana kushiriki katika kusambaza mdoli wa fowadi huyo wa Kinigeria aliyevalia rangi za klabu hiyo na maandishi “mshambuliaji” mbele.
Partenopei wametangaza kuwa watachukua hatua za kisheria dhidi ya watayarishaji wa toy hiyo, kwani hawakutoa kibali kwa mdoli huyo mwenye mfanano wa Osimhen, akiwa amevalia jezi ya Napoli.
Katika taarifa rasmi, klabu hiyo ilisema, “Kuhusiana na habari, ambayo ilionekana kwenye tovuti nyingi za habari za mtandaoni, zinazohusiana na uwekaji sokoni wa mchezo wa watoto unaoitwa ‘Cicciobello Bomber’ unaoonyesha sifa za mchezaji na Victor Osimhen, kwenye picha akiwa amevalia sare inayoonekana wazi kwa shati ya mchezo ya timu ya kwanza ya Klabu – SSCN inabainisha kuwa ni bidhaa isiyo rasmi, ambayo utambuzi wake haujaidhinishwa kwa njia yoyote na Klabu.
“Kwa hivyo Kampuni ilichukua hatua kulinda maslahi yake katika afisi zinazofaa.”