Klabu ya Yanga imeingia Mkataba miezi 18 wa udhamini na Karimjee Group kupitia kampuni yao ya pikipiki ya Hero ambayo ni Watengenezaji na wauzaji wa pikipiki za Hero nchini.
Mkataba huo una thamani ya Tsh milioni 300, Kampuni ya Hero yenye makao Makuu yake nchini India ilianzishwa 1984 na ipo katika Mataifa 40 Duniani ikishika nafasi ya kwanza kwa uuzaji wa Pikipiki Duniani.
“Leo tumeingia makubaliano na kampuni ya Karimjee Mobility kupitia kampuni ya Hero ambayo inatengeneza pikipiki na kusambaza. Kampuni ya Hero inatajwa kuwa kampuni namba 1 duniani kwa biashara hiyo. Kampuni hii kutoka India inafanya biashara mataifa zaidi ya 40. Young Africans SC itapata kiasi cha Tsh Milioni 300 kutoka kwenye mkataba huu katika kipindi cha miezi 18” Rais wa Young Africans SC Eng. Hersi Said
“Tuwahakikishie kampuni ya Hero kuwa sisi ni Klabu namba moja na tutahakikisha @heromototanzania ambao ni namba moja waendelee kubakia kuwa namba moja. Uwezo wa kuifanya Hero kuwa namba moja ni jukumu la kila Mwanachama wa Young Africans, hivyo kuanzia sasa bodaboda ni Hero” Eng.Hersi Said
“Mkataba huu utaruhusu kwa matawi yetu ya Klabu kupata posho kwenye mauzo ya pikipiki hizo. Kwahiyo kila tawi linapaswa kuhakikisha biashara hii inakuwa kwa kasi. Hivyo basi kila mwananchi pikipiki yako ya kununua ni Hero na pikipiki ya kutumia ni Hero” Eng.Hersi Said