Klabu za soka nchini zimeshauriwa kuwaamini wachezaji vijana ili kusaidia kupatikana kwa wachezaji wenye ukomavu na mashindano mbalimbali watakaoweza kuzitumikia timu za taifa za umri mbalimbali kwa miaka ya baadaye
Kwa nyakati tofauti wadau wa soka nchini wamekuwa wakikinzana juu ya idadi ya wachezaji wa kigeni kucheza nchini wengi wao wakidai idadi hiyo ipungue sababu ikiwa ni kutoa nafasi kwa wachezaji wazawa watakaoweza kuwa na ubora wa kucheza timu ya taifa pindi inapoitwa
Kwenye uzinduzi wa mashindano ya Safari lager uliofanyika Jumanne hii Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kusaka vipaji mikoani Kocha wa timu ya taifa chini ya miaka 20 Jamuhuri Kiwhelo anasema upatikanaji wa vipaji hivyo utakuwa hauna maana kama vijana wanaopatikana hawatapewa nafasi ya kucheza kwenye klabu zinazoshiriki ligi za madaraja ya juu
Kwa upande wake Mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga na Taifa Stars Sekilojo Chambua anasema mchakato huo wa utafutaji vipaji utasaidia kutoa nafasi kwa wachezaji wengi wanaoishi mbali na fursa ya kuonesha vipaji vyao
Baadhi ya wadau wa Soka Jijini Dar es Salaam wanaeleza uhitaji uliopo katika kuendeleza soka la vijana nchini