Ni siku kumi na tano zimepita tangu kuripotiwa tukio la vurugu katika mdahalo wa Katiba uliohudhuriwa pia na aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba Katiba Novemba 2 2014, leo katika Kikao cha Bunge Dodoma ishu ya walinzi kama wazee kama Warioba imechukua headlines kwenye maswali na majibu.
Akiuliza swali hilo Mbunge Moses Machari amesema; “…Majuzi hapa Mzee Warioba tunaelewa wote hapa Wabunge kwamba amefanywa nini pale Ubungo Blue Pearl Hotel.. Na hapo kwenye swali la msingi la Mheshimiwa Selasini limezungumzia suala la ulinzi kama umeliangalia swali hili, sasa waziri unaposimama na kulieleza Bunge kwamba wazee hawa wanajaliwa vizuri, mambo ya usalama yako sawasawa ni kutowatendea haki wazee hawa…”
“…Mawaziri ambao wanatoa majibu ya namna hii tunawafanya nini kwa sababu wanazungumza uongo ambao uko wazi, hili jambo ni suala la juzi.. Vinginevyo Mheshimiwa Kombani aombe radhi katika suala hili…”– Machari
Akijibu swali hilo Celina Kombani amesema “… Mimi ndiye Waziri ninayewatunza wazee, na ninachokisema nina uhakika nacho… Mzee Warioba anapata ulinzi kama walivyo wazee wengine.. na mfano mzuri mnamuona Mheshimiwa Lowassa hapa anapata ulinzi, Mheshimiwa Shamsi Vuai anapata ulinzi…”
“…Kwa hiyo wazee wastaafu wote wanapata ulinzi.. Unless kama ameacha walinzi wake… Nna uhakika na ninachosema analelewa, anatunzwa na ukitaka ushahidi nenda kamulize kama hapati facilities zote zinazostahili kwa viongozi wastaafu…”– Kombani
Kusikiliza swali la Mbunge huyo na jibu la Waziri Kombani, bonyeza play hapa.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook