Ikiwa ni zaidi ya miezi minne tangu Bomoabomoa ianze eneo la Kimara hadi Kiluvya Dar es salaam ili kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro, shughuli imefikia kwenye ubomoaji wa majengo mbalimbali ikiwemo Msikiti pamoja na Kanisa.
Imamu Mkuu wa Msikiti wa Masjid Kirumbi ambao unatakiwa kubomolewa ameongea na AyoTV na kusema “TANROADS wametupa wiki moja kubomoa huu msikiti ila mafundisho ya dini yanasema ni kosa kwa Muislamu kuinua mkono wake kuvunja nyumba ya Mungu“
“Wakisema TANROADS wavunje wenyewe ni sawa sisi hatuna ubishi lakini tunamuomba Muheshimiwa Rais atununulia eneo jingine, hatukatai kuvunja wala maendeleo ya nchi…. yeye mwenyewe alisema tumuombee, sasa tutamuombea wapi wakati Msikiti unavunjwa?“
Zaidi unaweza kujionea kwenye hii video hapa chini
UNATAKA KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI? Breaking NEWS, Za Mastaa, Siasa, Michezo na nyingine…. fanya jambo moja tu rahisi… BONYEZA PAGE ZIFUATAZO ili nikutumie kila kitu kiganjani mwako >>> INSTAGRAM <<<< FACEBOOK >>>> TWITTER >>> pia bonyeza SUBSCRIBE HAPA >>> YOUTUBE