Club ya Azam FC leo imeripotiwa kumsimamisha kazi kocha wake mkuu Hans van Pluijm na msaidizi wake Juma Mwambusi, ikiwa ni siku moja imepita toka ipoteze mchezo dhidi ya Simba SC kwa magoli 3-1.
Hans na msaidizi wake Juma Mwambusi wanafutwa kazi wakiwa ikiwa hawajamaliza hata msimu, tetesi za kuwa katika wakati mgumu kwa wawili hao zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Coastal Union game iliyochezwa Mkwakwani Tanga.
Azam FC inamfuta kazi Hans van Pluijm ikiwa ameiacha nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na point 50 imecheza michezo 25 sawa na Yanga SC wanaoongoza Ligi wakiwa na point 61 sawa na kuwazidi Azam FC kwa point 11.