July 15 2016 miongoni mwa habari zilizobeba uzito katika headlines za usajili wa wachezaji katika kipindi hiki cha dirisha la usajili ni kuhusiana na kiungo wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea Leicester City ya England N’Golo Kante ambaye anahusishwa na kujiunga na Chelsea.
Taarifa kutoka Skysport na baadhi ya mitandao mikubwa ya soka duniani, imeripoti leo July 15 2016 Chelsea kukubaliana na Leicester City dau la usajili wa Kante ambalo linakadiriwa kufikia pound milioni 32, Kante mwanzoni kabla ya Euro 2016 aliripotiwa kukataa ofa ya kujiunga na Chelsea ila sasa anaripotiwa kuwa weekend hii atafanya vipimo vya afya Chelsea.
Kante baada ya kufanya vipimo vya afya anaripotiwa kuwa atajiunga na Chelsea kwa mkataba wa miaka minne na baadae atasafiri hadi Austria walipoweka kambi Chelsea kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu England.
GOLI LA MECHI YA YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1