Leo June 1, 2018 Nakusogezea stori kuhusu Kwaya moja ya shule nchini Afrika ya Kusini ambapo imewashangaza wengi baada ya kudensi huku wakiwa watupu.
Waziri wa Elimu ya Msingi wa Afrika ya Kusini Angie Motshekga amesema amesikitishwa baada ya kuona kanda hiyo ya video inayoonesha kwaya hiyo ya Xhosa wakidensi huku wakiwa wamevalia vazi linalojulikana kama ‘Inkciyo’ na kudai kuwa kitendo hicho ni ukosefu wa heshima na kwenda kinyume na maadili na tamaduni za taifa hilo.
Kwa upande mwingine kiongozi wa Kwaya hiyo ametetea kwaya yake kwa kujinasibu kuwa wanaona fahari wakidensi namna hivyo.
Suala hilo sasa limewasilishwa katika idara ya kitaifa ya Motshekga kwa ajili ya uchunguzi zaidi na Waziri huyo aliongeza kuwa “hakuna makosa kupenda tamaduni na urathi (utamaduni ama desturi) wako lakini hakukuwa na haja yoyote kudensi wakiwa utupu”.