Leo May 28, 2018 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli, ameridhia uamuzi wa kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana.
Baada ya taarifa hiyo kutolewa aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye ameandika katika ukurasa wake wa Twitter Nanukuu “Pumzika Rafiki wa kweli, pumzika Mlezi na Mzazi usiyemfano, pumzika Kiongozi, pumzika Komredi. Mwalimu uliyebadili mtazamo wetu juu ya siasa na utumishi kwa umma! TUTAKUENZI DAIMA! Cde. Kinana! Umepanda mbegu na ITAOTA!”
Pumzika Rafiki wa kweli, pumzika Mlezi na Mzazi usiyemfano, pumzika Kiongozi, pumzika Komredi. Mwalimu uliyebadili mtazamo wetu juu ya siasa na utumishi kwa umma! TUTAKUENZI DAIMA! Cde. Kinana! Umepanda mbegu na ITAOTA! pic.twitter.com/e2rFLK8jIF
— Nape Moses Nnauye (@Nnauye_Nape) May 28, 2018