Kupitia NCA TV ya Afrika Kusini imeonyeshwa taarifa ya kanisa jipya lililopo nje kidogo ya Johannesburg ambalo Waumini wake pamoja na Askofu wao wanakunywa pombe huku ibada ikiendelea.
Askofu mkuu wa kanisa hilo lijulikanalo kama Kabhula, Askofu Itiehth Makiti ameeleza kuwa lengo kuu la kanisa hilo ni kuwapokea watu ambao wametengwa na kukataliwa na jamii zao au Makanisa yao kutokana na tabia zao za kunywa pombe.
Ameeleza kuwa yeye kama kiongozi wa kanisa hilo analiongoza kwa kuonyesha mfano na hivyo hata yeye mwenyewe kabla ya kuanza kuongoza ibada anakunywa kilevi anachokipenda ambapo Waumini wapya hukaribishwa kwa maombi na kunyweshwa aina ya pombe wanazozipenda…. tazama zaidi hapa chini
Ulipitwa na hii? Makonda amjibu Wema baada ya kumuandikia “Sikukufahamu mpaka nilipokuchukia”