Hakuna mtu anayependa wizi kiukweli, ikitokea mwizi amekamatwa mara nyingi watu hujichukulia Sheria mikononi kutokana na hasira za kuuchukia uhalifu.
Hii kutoka Kenya, wakazi wa eneo la Laare Kenya wamejiwekea utaratibu wao, wamesema ikitokea wamekamata mwizi yoyote wanamkata mkono, wanaamini kwa hii njia wizi utakomeshwa.
“Rais alisema ulinzi unaanza na wewe sasa kama uko na kitu yako hufai kunyang’wanya kitu yako.. na kama mtu akikushikisha ukuta unachukua hatua wewe peke yako”; Hapa amenukuliwa mmoja ya wakazi wa eneo hilo.
Watu wa eneo hilo wamesema sime imekuwa silaha muhimu kukamilisha zoezi hilo huku wauzaji wa mapanga wakifurahia kupata wateja wengi wanaonunua silaha hizo.
Wapo watu ambao wamejiwekea utaratibu wa kutembea na sime zao kwa tahadhari ikitokea wakati wowote mwizi kakamatwa.
Nimekuwekea sauti niliyoirekodi kituo cha K24 wakati taarifa hiyo ikiruka hewani.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook