Baada ya kutoka kwa video kwenye mtandao wa alkataib wanamgambo wa kigaidi wa alshabaab watekeleza ugaidi nchini Kenya na kuwaua watu watano katika miji ya Nairobi na Mombasa nchini Kenya.
Mei 3 majira ya saa 2 usiku milipuko miwili yalitokea kwa mpigo Mjini Mombasa moja katika eneo la Nyali hoteli ya Reef iliyomuua mtu mmoja na nyingine eneo la kituo cha mabasi cha Mwembe tayari .
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kwamba mtu aliye kua katika gari aina ya Toyota Probox Alirusha bomu kuwalenga wasafiri walio kua wakisubiri kufika kwa basi.
Bomu hilo lililokua ndani ya mkoba kilicho kua kimetelekezwa ufuoni mkabala na hoteli ya reef kililipuka katika eneo la lango lilipokua likikaguliwa na walinzi baada ya mtu mmoja kukiona na kukisalimisha kwa walinzi akidhani mwenyewe amekisahau.
Jumapili Mei 4 jiji la Nairobi watu 3 waliaga dunia na wengine 60 walijeruhiwa baada ya kutokea milipuko miwili kwenye mabasi mawaili tofauti katika barabara ya Thika super Highway jijini humo,mlipukohuo unasemekana ulitokana na vilipuzi vya IEDS vilivyokua vimewekwa katika mabasi hayo yaliyo kua yakiwasafirisha watu kutoka katikati mwa Jiji.
Taarifa kutoka maafisa wakuu wa polisi na mashuhuda wa matukio hayo wamesema kwamba mlipuko wa kwanza ulitokea saa 11 jioni karibu na eneo la homeland ambapo basi la Jeean Sacco lililipuka likiwa linaeleka Githurai 45,tukio la pili lilitokea dakika kadhaa baadaye katika mzunguko wa Roysambu katika basi la Mwi sacco lilokua na abiria 51 waliokua wakisafiri kwenda mwiki.
Hadi sasa wameripotiwa kufariki kwa watu 6 kufuatia shambulizi dhidi ya mabasi mawili jijini Nairobi na wanne Mombasa,baada ya shambulizi kwenye kituo cha mabasi mwembe tayari na katika hoteli ya Reef kule Nyali.
Kenya imekabiliwa na zaidi ya mashambulizi 80 na watu 300 wamefariki tangu wanajeshi wa Kenya kuanza kuwakabili wanamgambo wa Alshabaab kule Somalia.