Mwezi December 2014 kulikuwa na story ya mtuhumiwa mmoja kuuawa kwa kupigwa risasi wakati alipokuwa akijaribu kutoroka Mahakama ya Kisutu kwa kuruka ukuta wa Mahakama hiyo, story kutoka Kenya leo inafanana na hii.. inahusu mtuhumiwa mmoja kufanya jaribio la kutoroka kutoka Mahakama ya Machakos.
Mtuhumiwa huyo alijaribu kutoroka lakini askari wakampiga risasi mkononi na mguuni akiwa juu ya ukuta, majeraha hayo yalimfanya ashindwe kukimbia, akakamatwa.
Mahabusu huyo alifikishwa Mahakamani kwa kosa la kufanya vurugu baada ya kulewa na hukumu yake ilikuwa alipe faini ya Kshs 200, jaribio lake la kutoroka limefanya awe na kesi nyingine mpya kutokana na kufanya kosa hilo.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook