Kocha wa Inter Milan Simone Inzaghi ametia saini mkataba mpya utakaomweka klabuni hapo hadi 2025, timu hiyo ya Serie A ilisema Jumanne.
Mtaliano huyo mwenye umri wa miaka 47 alianza maisha yake ya ukocha katika Serie A Lazio kabla ya kujiunga na Inter mwaka wa 2021. Mkataba wake wa sasa na Inter ulikuwa unakamilika mwishoni mwa msimu.
Inzaghi aliiongoza Inter kutwaa mataji ya Coppa Italia katika misimu ya 2021-22 na 2022-23, Supercoppa Italiana 2021 na 2022 na fainali ya Ligi ya Mabingwa ya mwaka huu, ambapo walipoteza kwa Manchester City.
“Inter Milan ina furaha kutangaza kumuongezea mkataba kocha Simone Inzaghi. Shukrani kwa makubaliano mapya, kocha atakuwa kwenye usukani wa Nerazzurri hadi 2025,” Inter ilisema katika taarifa.