Mwanamuziki nguli wa mtindo wa Rumba ya kutoka DRC, Koffi Olomide amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela kwa kuwateka nyara wachezaji wake wa zamani.
Koffi, ambaye jina lake halisi ni Antoine Christophe Agbepa Mumba, hakuwepo mahakami wakati hukumu hiyo iliposomwa Jumatatu Desemba 14, na mahakama ya Versailles, nchini Ufaransa.
Katika kesi ya awali Koffi alituhumiwa kuwanyanyasa kingono wasichana wanne waliokuwa wakicheza katika bendi yake Quartier Latin lakini mashtaka hayo yalifutwa na katika kosa la utekaji nyara pia atatakiwa kulipa euro 72,000 kama faini ambazo zitagawanywa kwa waathirika.