Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo amesema kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya mitandao nchini zimetokea changamoto mbalimbali za viashiria vya matishio ya kuhatarisha usalama na usiri wa taarifa. Dkt Sasabo ameeleza hayo leo July 12, 2019 wakati akifungua mafunzo ya usalama mtandao yaliyoshirikisha taasisi mbalimbali za kiserikali nchini.
‘’Kwa kuwa utandawazi haujali mipaka ya nchi inabidi tuwe makini na tujipange kukabiria na viashiria au matukio hatarishi endapo yatatokea kwa haraka, nimeambiwa kuwa hili ndio lengo kuu la mafunzo ambayo yatatolewa kwa kipindi cha wiki nzima”-Dkt. Sasabo
MTANZANIA ANAEFUGA MENDE “MMOJA NAUZA Tsh.1000, SOKO NI KUBWA MPAKA NAPAGAWA”