August 31, 2019 Msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi katika Serikali ya awamu ya tano mbele ya Waandishi wa habari Dodoma, aliulizwa hatua iliyofikiwa hadi sasa ili kuinusuru ndege ya Tanzania inayoshikiliwa nchini Afrika Kusini pamoja na baadhi ya Watanzania kuhusika kuihujumu ambapo katika majibu yake Dkt. Abbasi amesema sio vyema kwa sasa kuendelea kulizungumzia jambo hilo ambalo bado lipo Mahakamani.
“Nachelea sana kutokuingia sana kwenye huo mjadala kwasababu ni kesi ambayo tayari ipo Mahakamani lakini niseme tu tusubiri uamuzi wa Mahakama maana naweza nikaongeza ya kwangu hapa hivyo sipendi kuingia sana huko”- Dkt. Hassan Abbasi
MKUU WA WILAYA ALIETAKA KUUAWA AZUNGUMZA “AROBAINI WAMEKAMATWA”