Mbunge wa Mbinga Magharibi John Komba Novemba 6 2014 alikua miongoni mwa waliosimama na kuwasha kipaza sauti kwa ajili ya kuzungumza kwenye kikao cha Bunge ambapo aliyazungumza haya…
1- Kuhusu kauli ya Mbunge Peter Msigwa juu ya Katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana; “..kwa kuanza kwanza ni.. sikupenda sana kwa hotuba aliyoitoa mwenzetu Msigwa jana kuhusu katibu wetu mkuu Kinana wa CCM.. nataka nimuhakikishie Msigwa.. kati ya makatibu wakuu tuliowapata katika Chama cha Mapinduzi..waliokifanyia vizuri chama chetu cha mapinduzi… Kinana ni miongoni mwao na ndio tishio la upinzani kwa sasa hivi.. Kwa hiyo kumuingiza Kinana pale kumletea maneno ambayo hajayasema.. ni kiwewe tuu cha buree cha bure.. Kinana yupo pale kuwaondoeni nyie mnaosema mtachukua nchi…”—Komba
2- Kuhusu alichofanyiwa Jaji Warioba; “.. Pili nitoe pole kwa mzee Warioba.. juzi yale yaliyompata pale siyo jambo jema.. na yeye anasema kwamba hayajawahi kuona tangu uhuru.. lakini angesikia ushauri wangu wakati ule wa Bunge la Katiba haya yasingetokea.. akae tuu pembeni .. aache mjadala wao uendelee kama kawaida na utaratibu uende kama kawaida yeye alimaliza kazi yake.. wengine wafanye kazi yao na katiba hii mwisho ipatikane nzuri.. ukiingilia ingilia hayo ndiyo yatakayokupata.. mzee pumzika tuu…”– Komba
Ukitaka kuisikiliza sauti ya Komba akizungumzia hayo leo Novemba 6 kwenye kikao cha Bunge, iko hapa bongyeza play.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook