Taarifa kutoka eneo la eneo la Kiamaina, Nakuru mtu mmoja amekamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi baada ya kukutwa akifanya mapenzi na kondoo.
Mtu huyo aliyetambulika kwa jina la John Chege mwenye umri wa miaka 27, ambaye ni fundi wa kukarabati mabomba ya maji katika eneo hilo amekiri kufanya kosa hilo japo amelalamika kuwa mama yake mzazi amehusika kumuandalia mtego wa kumkamata akifanya kitendo hicho kwa lengo la kumuaibisha.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa watu walioshuhudia kitendo hicho wamesema mtu huyo alitumia dawa za kulevya kabla ya kufanya kitendo hicho.
Kamanda wa Polisi tawala kata ya Kaonti, Moses Lekakeny amesema mtuhumiwa huyo atafanyiwa uchunguzi na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.