Urusi inaweza kutarajia Korea Kaskazini kuiuzia makombora mapya zaidi katika miezi ijayo, waziri wa ulinzi wa Korea Kusini amesema.
“Korea Kaskazini, ambayo inahitaji pesa, inauza kikamilifu silaha mpya ambazo Urusi inataka,” Shin Won-sik aliambia tovuti ya Yonhap.
Pia alisema Korea Kaskazini inaweza kufanya majaribio zaidi ya silaha – ili kuzidisha hali ya wasiwasi kabla ya uchaguzi wa Korea Kusini na Marekani.
Raisi Shin alitoa mfano wa ziara ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wiki hii katika viwanda vya kutengeneza silaha, ambako alikagua kile kinachokisiwa kuwa makombora ya masafa ya karibu yaliyotengenezwa hivi karibuni – yenye uwezo wa kubeba silaha za kinyuklia.
Hayo yamejiri huku takriban nchi 50 zikilaani ununuzi na matumizi ya Urusi ya makombora ya balistiki ya Korea Kaskazini dhidi ya Ukraine.